Habar za siku tele ndugu zangu, naomba nichukue fursa hii kuwapa habari kidogo juu ya jambo hili. ni kuhusu uwepo wa nafasi za kazi na idadi ya waombaji wa hizo nafasi. hivi juzi juzi shirika moja maarufu hapa nchini lilitoa nafasi kibao tu za kazi, kwa mujibu wa chanzo changu cha habari wanaohitajika ni kama watu thelathini hivi, lakini ugumu unakuja hapa, waombaji wa hizo nafasi ni zaidi ya elfu kumi(10,000).
sasa kwa wenzangu na mimi ambao ndo kwanza tumemaliza vyouni nadhani ni kiasi gani tunavyoona mtaani palivyo pagumu.binafsi nashauri kwa wanzangu wengi tubadili muelekeo wa maisha yetu kwa mtazamo chanya na kuelekea aidha katika kilimo, kufuga au ujasiriamali kwa ujumla. kama tutajiweka katika makundi ya watu japo watono au kumi tunaoaminiana naimani tutafanya mambo makubwa na kuweza kufika mbali badala ya kukaa na kutegemea kuajiriwa ambapo idadi yetu imezidi ajira zilizopo zaidi ya mara 80.
kuna taasisi nyingi zimekuwa na tabia ya kutumia muda na nguvu za watu wedngi kwa ajili ya manufaa yao wachache, kuna watu wameshawishika kuingia katika biashara za mtandao ambazo matokeo yake zinawagharimu kwani mwisho wa siku waliotangulia kuingia katika hizo program ndo wanafaidika zaidi, binafsi siwashauri wenzangu muingie katika mitego ya namna hiyo. si vizuri kuzitaja hizo taasisi zenyewe hapa ila kama mtu atahitaji tuwasiliane nami ntamtumia majina yake.
Ikumbukwe kuwa KAZI hazitafuti watu ila watu ndo wanatafuta kazi, na kupata kazi ni KAZI kama neno lenyewe.
Niwatakie kila la kheri na tuwe makini zaidi.

No comments:
Post a Comment