Monday, November 28, 2011

Shule tumemaliza, vp kuhusu ajira?

hi again my dear viewers, habar za maisha? like the topic says, we have completed our studies( the colleges and university thing, what about getting employed?) nadhan hilo ni swali ambalo wengi tunajiuliza hasa tukizingatia jinsi tulivyokuwa tukijipa moyo tukiwa mashuleni kwamba as soon as we finish our studies there will be plenty jobs waiting for us to fill them, inavunja moyo but ndo ukweli wenyewe kwamba kazi ni chache sawa na hakuna kabisa, so what to do? tujiajiri, tutafanyaje bila kuwa na mitaji ya kuanzia(capitals to initiate), nani ni mkarimu kiasi cha kutusaidia ili tunyanyuke nasi tuwe katika maisha mazuri, ni biashara au shughuli gani ya kufanya ili itukomboe? binafsi maswali haya yananiumiza kichwa saana, inafika kipindi najiuliza " is it worth it" the time i have wasted and resources spent? kweli inabidi tubadilishe system za maisha yetu kwan maisha yamesha badili muelekeo wake na kama hali itaendelea kuwa hivi ni wazi kwamba degree moja si kitu tena labda kwa wachache wenye bahati na waliokuwa ktk channel nzuri.

mwaonaje wenzangu? until next time adios! 

Wednesday, November 16, 2011

Taarifa kuhusu Kazi na waomba kazi

              Habar za siku tele ndugu zangu, naomba nichukue fursa hii kuwapa habari kidogo juu ya jambo hili. ni kuhusu uwepo wa nafasi za kazi na idadi ya waombaji wa hizo nafasi. hivi juzi juzi shirika moja maarufu hapa nchini lilitoa nafasi kibao tu za kazi, kwa mujibu wa chanzo changu cha habari wanaohitajika ni kama watu thelathini hivi, lakini ugumu unakuja hapa, waombaji wa hizo nafasi ni zaidi ya elfu kumi(10,000).
                sasa kwa wenzangu na mimi ambao ndo kwanza tumemaliza vyouni nadhani ni kiasi gani tunavyoona mtaani palivyo pagumu.binafsi nashauri kwa wanzangu wengi tubadili muelekeo wa maisha yetu kwa mtazamo chanya na kuelekea aidha katika kilimo, kufuga au ujasiriamali kwa ujumla. kama tutajiweka katika makundi ya watu japo watono au kumi tunaoaminiana naimani tutafanya mambo makubwa na kuweza kufika mbali badala ya kukaa na kutegemea kuajiriwa ambapo idadi yetu imezidi ajira zilizopo zaidi ya mara 80.
              kuna taasisi nyingi zimekuwa na tabia ya kutumia muda na nguvu za watu wedngi kwa ajili ya manufaa yao wachache, kuna watu wameshawishika kuingia katika biashara za mtandao ambazo matokeo yake zinawagharimu kwani mwisho wa siku waliotangulia kuingia katika hizo program ndo wanafaidika zaidi, binafsi siwashauri wenzangu muingie katika mitego ya namna hiyo. si vizuri kuzitaja hizo taasisi zenyewe hapa ila kama mtu atahitaji tuwasiliane nami ntamtumia majina yake.
             Ikumbukwe kuwa KAZI hazitafuti watu ila watu ndo wanatafuta kazi, na kupata kazi ni KAZI kama neno lenyewe.

Niwatakie kila la kheri na tuwe makini zaidi.

Saturday, November 5, 2011

Ndugu zanguni

habari za majukumu?
ni matumaini yangu mabo c mabaya saana kwani waswahili wanasema "bora uzima" sasa ningependa nichukue fursa hii kuwashauri wenzangu na mie ambao bado hatuja pata ajiri rasmi, kujiajiri wenyewe aidha kwa kujiunga au kuanzisha vikundi vyetu vya ujasiriliamali kwa kipato kidogo cha kudunduliza tunaweza fanya mambo mengi, kama una access na internet au una email, tuwasiliane kwa email kwani nna mengi ya kujulishana hasa upande wa ujasiriliamali, ingawa wazo langu la mwanzo ilikuwa ni uhasibu na ugavi, inanibidi ni diversify ili kukidhi hali ya sasa ya kiuchumi. tuwasiliane jamani kwani nna mengi ya ku share pamoja. kwa sasa nimeshakuwa affiliate marketer wa kampuni mbali mbali, nna imani sote tunaweza fanya japo kwa uchache nasi tukapata japo kiasi kidogo cha fedha za kujikimu na matumizi madogo madogo, hakuna gharama kama za kuhudhuria street university ya erick shigongo, muhimu tufatiliane kwa umakini zaidi.

all the best.